Africans working in Gulf share stories on what they go through daily,Mwaisha kwa mwarabu

by venas
10 views

Here are the stories of Kenyans and other Africans shared on what they go through in Arab countries:

“”Unaenda kushtaki mtoto wa mwarabu kwa mamake, unapate mamake anatema kikohozi kwa sink Iko na vyombo, unaenda kwa babake nae unapata amekanyaga carpet ya white yenye umeosha na haijakauka, unachil unaenda kuambia kijana nae Sasa amenyonga tissue ziko Kila mahali vinyasa zimejaa mavi🤦🤦🤦 inabidi tu Sasa ukumbuke shida zako na utulie”

Another one said:

“Pads whether used or not sichukui.. dirty panties sifui wee fua nitatoa kwa drier, tema mate kwa kila sink ya hio nyumba buh keep off my sink ya kitchen, make sure choo yako ni safi before niingie kuosha…mahali utaacha manguo hapo ndio utaokota ata kama ni after mwaka moja…mambo ya kupika niachie ..sikulangi ata kwa mamke madam mimi..chakula ya waiguru siwezi kula ndio nikaamua kupika…nyumba naosha once kwa siku na usiku wakilala..nguo nkipanga upangue utazivaa hivo adi miezi mbili khalas…ukiona sifanyi kazi mzuri jib shagalla thania ana mafi punda mashugula kuliom kuliom..wakat nom mafi ahad ndungini bab…mafi shugul ana nom adi nitosheke…mimi nayo kibarua nachapa kama hakuna kesho then God’s grace on top napendwa kama sizz wa hii nyumba alhamdulilah”

Another one confessed:

Hawa watu wengine hukua wachafu sana,choo hawaflash,mswaki akipiga Kwa sink hamwagii maji hiyo uchafu,nguo ziko na periods zinawekwa hivyo..umemop nyumba mtu anakuja ku blowdry nywele sitting room anawacha nywele Kila mahali 😏,ikija Kwa watoto utalia wasumbufu sana.. watoto wakubwa ata wengine mnatoshana ATI akienda shule lazima umuamshe asiachwe na bus ..wewe ndio alarm Yao..unaamsha mtu anakataa kuamka na alijiwekea alarm anawachwa unagombanishwa..unaskia kumkula makofi😂. nilikua na mwengine wa 6years ATI umbembeleze ndio aoge,kubrush,akule sijui kumchanua nywele mara umbebe kama mtoto aii niliwauliza kwani ni mtoto mchanga Kenya mtoto wa 6years anajifanyia vitu mob..then kukawa na mwengine about 13 years but alikua na ugonjwa sijui leukemia or whatever but naskia ndio alikua anapona Yani anabehave kama chizi..ukimwamsha aende shule mnapigwa mawe nyumba nzima mara asishoutiwe..ukifanya kazi umalize anakuja na jug ya maji anamwaga Kwa sitting yote..ukipika mboga kwanza anabeba anaenda kula kitambo upike rice inaliwa tupu unateteshwa ATI unaharibu food ju watashikashika coz Haina mboga so unamwaga..salary ukilipwa after 2days ATI uwakopeshe hiyo pesa yako hawana yakutumia..nilivumilia 6 months nikaona depression itaniua vile nilitoka nikarudi home ata hawakuamini kama ni Mimi niliwatenda..nilingoja watoto hawajaenda shule so wakapelekwa hosie ndio waandikiwe sick sheet kuonyesha ATI walikua wagonjwa na ni uongo walichelewa gari ikawaacha so lazima barua ndio wapeleke shule..vile walitoka na Mimi the previous 2 days before nilikua nimeachwa na safe haikua imefungwa mahali walikua wameficha pp yangu nikaitoa na nikarudisha funguo nikawa nishapack..walipoenda ikakaribia lunch nikajua wako karibu kurudi nilikua nitayarishe lunch na nilikua nimeachwa na huyo chizi wangu..nilimwacha akiangalia TV nikatoka na virago zangu nikajipeleka deportation center ju nilikua nishajua pale Iko.. after 2weeks Mimi huyo Kenya ata sikutaka kujua wako na pesa yangu.. nilifika Kenya nikaambia mungu asante ata kama sikuja na pesa but I was safe.. kufungua simu napata nimetumiwa👹..nilicheka ju walikua wanaona Niko mpole wakiteta nanyamaza siongei ama na smile ATI huyu ni mzuri..we want you to stay with us forever 😄nilisema nijikute..hiyo nyumba niliona moto na agent nao hukua hovyo ukiwaambia unateseka wao hukuambia vumilia umalize 6 months.kumbe ni vile 3months hua probation na ukitoka within that period atalipa mtu akureplace but ukimaliza 6 months na uhepe contract imeisha yake na huyo boss ju itabidi boss agaramike kulipa ndio apate mwengine..

Related Stories

Total
0
Share