This is How Nyota Ndogo is Suffering-This is Too Much From Her Family

704

Celebrated musician,Nyota Ndogo,has revealed how she is suffering in the hands of her family.The former house girl has gone public to explain how ungrateful her family is even after she has done everything to make them happy. Here is her story

PART 1

Kitambo nikianza mziki nilikua muoga sana.nilikua naogopa sana magazeti.nilikua nikiskia nipo kwenye gazeti naanza kulia maana najua nimetukanwa sana umo ndani.hamuezi kuamini familia yangu ilitake advertage of that.walijua huyu anaogopa sana media kwaivyo tukimwambia chochote atafanya.mimi nimekua nikimuangalia mama toka nafanya kazi ya nyumbani na senti zangu kidogo but zote nitampelekea mamaangu kwakua sikua na maitaji .nilikua najinunulia always mafuta yakujipaka tu kila mwezi hela zengine kwa mamaangu.couse nilikua najua kuna wadogo zangu kule nyumbani ambao pia wanaitaji msaada.ok mimi sio wa kwanza kwa familia kuna mkubwa wangu ambae uwa sijawai kumuongea hata siku moja but aliwai kuji introduce mwenyewe siku ya harusi yangu kwa MATUSI nafkiri munamkumbuka kwakua mimi nikiwa mfanyikazi wa nyumba yeye alikua tayari ni mwanamziki na nilipomfata na nyimbo zangu anisaidie aliniambia siwezi kuimba na sikuwai kumfata tena.kwakua nilikua nakaa kazini miezi minne kabla kwenda nyumbani nilitafuta njia za studio na nyote munajua nilifika vipi studio.nilirekodi ulbum bure kwakusaidiwa.nyimbo zinapigwa kwenye radio mimi bado nafanya kazi ya nyumba.siku naenda kumuona mama namwambia mama mimi naimba kuna nyimbo zangu zachezwa kwa radio mama akafurai.kaka hakujua ni mimi.aliponiona akaniambia kuna mschana anaimba kweli umesikia? Anaitwa nyota ndogo?.nikamwambia huyo nyota ni mimi.so hakunisaidia na chochote kimziki wakati alikua uwezo anao.na kuona kua nyota kaenuliwa na watu wa nje na sio yeye na nyota anavuma kumliko yeye hapo ndip chuki alipoanzia.ananichukia miaka yote amekua akiniambia mziki wangu hauendi popote toka naanza.chuki ya kwamba aliwai kunipiga mimi na unyota wangu hadharani mbele ya watu mtaani kuniaibisha tu kisa kumtuma dadangu dukani kuleta chumvi kaleta tomato nikamwambia rudisha sujakutuma hicho yeye akaanza kuniambia unaringa kwakua unapesa.nikamuuliza pesa gani nilizonazo akaanza kunipiga………

PART 2

Sasa kama kuna kitu uniumiza zaudi yani hamuezi kuamini ni mamaangu.tupo madada wa nne wavulana wawili.nimefanya mengi mpaka kujisahau mimi mwenyewe kujiangalia.nipo na dada anaenifata nafkiri mulimuona anaitwa leila.mimi nalela tupo na tabia tafauti sana.mimi nimemchukua mtoto wa leila wa kwanza yupo mikononi mwangu.tukirudi nyumba wakati naishi mtopanga.kuna wakati mamaangu alikua anaishi sehemu inaitwa jua kali kuna nyumba za udongo kule hazina stima wa maji.nyumba ile nilikua nailipa elfu tatu but nikawa na mwambia mama tafuta nyumba nzuri sisi tushirikiane tuchange tulipe rent yako.juma akasema muache aishi anavyotaka uwezi kumcontrol mama aliekuzaa but kiukweli alikua anahepa ule mchango kwaivyo kwake yeye ni sawa mama akiishi kwa nyumba ya aina ile wakati tunajua tukishirikiana tutalipia nyumba.pia watu walikua wakinisema vibaya eti mamake nyota anaishi kwenye mazingira ya ajabu wakati amevuma.ukimuona mama kachoka nguo anazo vaa yani uwezi kuamini ni mamake nyota but hata nimnunulue nguo mama anauza yani mamangu uniliza mimi.ujitembeza kama mwenda wazimu watu wananisema mimi na sio kwamba hana but ni yeye mwenyewe ila mie yaniumiza kwakua watu hawaelewi na kutembea ni hadharani so kila mtu anamjua.so juma hajali mama anavyoishi couse hakuna siku watu umuita mamake jumaa.watu umuita mamake nyota.na juma hajali jina langu likiaribika yeye anafurai.kwaivyo niligoma kuilipa ile nyumba nikasema silipi hii nyumba labda ahame aende atafute nyumba nzuru juma akasema mimi nitalipa.so akawa anailipa yeye ile nyumba ya mama yani yeye hana neno mama akiishi kwenye mazingira yale.sasa siku moja nikamuamisha mama aje akae jaribu na mimi mtopanga.nikamkodishia room nzuri kama kawaida ataishi na leila na pili na watoto wao.nikifanya shooping kwangu nyumbani nitafanya na kwa mama vile vile masister wamekaa tu hawafanyi chochote mimi ndio niwaangalie nyumba stima maji na chakula.na hamuezi kuamini nilikua nikifanya hivyo.nakumbuka kuna wakati nilitoka show.nikaenda dukani nikanunua gunia la mchele sukari kilo kumi maharage kilo ishirini gunia la makaa.nikapeleka kwa mama but sikumkuta nikampata leila na pili.nikawaambia basi jamani tafteni hata kabiashara kadogo.

PART 3

Nikawaambia mukifanya kabiashara kadogo hata mama mutampumzisha couse yeye anafaa apimzike sisi tumuangalie yeye sie yeye awataftie nyinyi na watoto wake.sasa niliwaambia tukiwa chumba pole pole.mama alipokuja jioni sijui walimuambia nini.mama alikuja kwangu na hasira alinitupia maneno mazito sana.kwanini umekuja kwasomea wenzako barabarani kwasababu ya chakula ama kwakua unajiona wewe uko nazo wenzako hawana.nililia sana nikamwambia mama hata uniulizi yani ulioambiwa kwako tosha?akaniambia upo na roho mbaya sana mamangu mzazi aliniambia huyo MUNGU aliekupa ndio atakae kupokonya siwezi kusahau nikasema mama unanilaani mimi mama yani mama unanilaani mimi nilibeba majukumu yako yote nililia sana.kilichofatia niliita vijana wawili wa mtaani nikawaambia naomba twendeni kwa mama tukachukue kile chakula tulichopeleka tupeleke nyumba ya mayatima na yes tulichukua nikapeleka nyumba ya mayatima nikasema hawa watanishukuru kuliko kule kwa mama.wakati juma aliponitukana siku ya harusi hakutosheka.wakati nafanya subira yangu tour akaanza kunitumia ujumbe kua nitatangaza ulimnunulia mamako chakula kisha ukampokonya.sikumjibu iwapo atatafu kitu cha kusema ndio hicho.kuna wakati nilisafiri kwenda zanzibar kwenye festival tulikaa siku nne kule.niliporudi nikakaa kwangu siku tano sikumuona mama mdogo wangu akaniambia mama uwa analala kwa vibaraza kule mombasa nyumba alimuachia leila na boyfriend yake.mwanamume alie mzalisha.kwaivyo nani atalipa hio nyumba nikauliza.nikaambiwa vile ulimchukulia mama utabidi uendelee kulipa kwaajili ya mama.kwaivyo nilipe nyumba anayo ishi leila na bwana.kisha kila siku watakuja kwangu tusaidie na unga chumvi sukari hatuna hivi hatuna vile ukisema huna waambiwa waringa.mimi nakumbuka nikiwa na mimba ya mbarak dadangu laile alikua akiniona njiani ananitemea mate..nilijikuta siendelei nipo pale pale.pesa nashika nzuri kwa mziki but hakuna la maana kila kukicha watu wanataka niwaangalie wao tu na watoto wao.na mamangu ndio uwaonyesha kua mwanaisha anaweza kuwafanyia.mukitaka kujua mamaangu hanijali hakuja harusi yangu kwanini? Ukimuuliza atakwambia jumaa alinifungia mlango oh jumaa alikua ananifata mpaka chooni ili nisije harusi.

Hivi kweli mtoto anaweza kumcontrol.mama kweli.so wapenzi wangu mimi mpaka leo uwa ninauchungu na mamaangu uwa na mwambia kila siku hanipendi.akiwa na juma ataniponda vibaya sana.akiwa na mimi atamponda juma sana na akiwa na wale wengine ananiponda zaidi.niliwai kumkuta mamangu na juma siku moja wakiniswngenya wakati nimekwenda kumtembelea mama kwa juma alikua amekwenda kumtembelea nairobi na mimi nilikua nimeenda kimziki.nilisimama mlangoni nilikua napondwa mimi machizo yanitoka hawajui nipo hapo.nilipojitokeza walishtuka sana kuniona.nilikua nalia siwezi kuongea but nakumbuka neno nililo mwambia mamangu ni mum haina shida yote umeyasema nimekusikia but nakuakikishia huyu ambae ndio kipenzi chako hakuangalii kama mimi na sina ila nakuakikishia kwa uwezo wa MUNGU nitakujengea nyumba bila usaidizi wa mtoto wako yoyote.sina uwezo saizi but ninaimani na nikaondoka.uwezi kunilazimisha mimi nimlipie dadangu na mume wake nyumba na niwafanyie shooping.siku moja leila alienda kwenye radio moja ambapo kuna mtangazaji moja wa hio stesheni alikua hanipendi kabisa.leila alienda pale akapewa mda wa masaa mawili kunipondo on air.dada alikwenda kuniongea vibaya kwa radio kua nimetupa famili simsaidii mama sijui nipo na maringo kwakua nipo na pesa.dada moja akanipigia simu kuniliza kama naskiza radio mda uo.nikasema hapana naendesha gari naenda malindi sijawasha radio.akaniambia stop mahali washa kuna kipindi.nilistop nikawasha namsikia dadangu anavyoniponda niliishiwa na nguvu mwili mzima mimi hata sijui kwanini sijapata ugonjwa wa moyo yani ni MUNGU ananilinda.nikampigia juma simu nalia wakati huo kwakua yeye ndio mkubwa aonge na leila.aliniuliza sasa mimi ni fanyeje? Yani vile nilivyokua nalia hakujali kabisa kuja kujua kumbe alikua anafurai kua naaibishwa hata kama ni kwa uongo.sasa niwalete kwa haya hivi karibuni.harusi mpaka kumjengea mama.

Niliamua kuondoka mombasa kwaajili ya familia yangu.nilikua na stress kibao nilimchukua my son mbarak kuondoka mombasa kuanza maisha mapya kwengine na yes nilikua na mtoto wangu pekeangu na mama wa kazi.mbarak was only 4years then.nikaja voi.ndio niaanza kufikiria kuhusu kujenga nikanunua plot nikiwa tu pekeangu.nilikaa sana single kabisa couse uwa sina haraka ya waume.nikashikana na kijana moja but sio voi but nairobi tu.sikumchunguza vizuri nikashika ujauzito wa barka jamaa akaniambia yeye alikua ana mke but walikua wametengana famili imewarudisha pamoja kwakua huyu mke amejifungua.sasa mimi na mwambia mie mja mzito yeye ananiambia mke wake kajifungua.nikamwambia nilihapa toka mdogo sitawai kutembea na mume wa mtu.ulinidanganya wacha itoke hivyo hivyo.imagine watoto wawili pekeako singlie mum na huku nalipa nyumba yangu na huku nalipa ya mamaangu but hakuna hata siku moja mbarak amewai fukuzwa shule kwaajili ya fees wala sijawai kufukuzwa nyumba couse nyumba nilikua naweza kulipa hata 7months ndio nijipange na mambo mengine.hakuna mtu wa familia aliwai kuniuliza ujauzito niwanani ila nakumbuka niliwai kumpeleka kwa juma one day but hawajui chochote kumuhusu.mimi nimejifungua mbarak hospitali mamangu anakuja kama mgeni naoshwa na watu wa nje naletewa chakula na watu wa nje naudumiwa na watu nje mamangu hajawai shtuka na mimi kabisa.but wacha mke wajumaa ajifungue.atenda nairobi mpaka mtoto atambae ndio arudi.so ndio hivyo ni kama sina mama.

So familia ilijua nakuja na mume na walijua ni mzungu.tulikua tuende kwenye saa tano hasubui ndio tukae mpaka jioni tukitia story.kwaivyo nilijua wanajua tunaenda na tutapikiwa lunch but kitu kikaniambia hebu mpigie tatu simu ujue kukoje uko kwa juma maana ndio tuendako.nikamoigia simu nikamwambia twaja sisi couse tatu ndio dada pekeake anaenielewa na anaejua kurudisha shukrani.tatu akaniambia mwanaisha sitakudanganya juma amesema tuapikie chapati na maharage.nikasema what? Akasema hata vyaelekea kuiva hivi njooni tu.nikasema mimi sina shida na maharage but mgeni jamani.nikamtumia tatu pesa nikamwambia nunua nyama kilo nne kaanga kando imagine na akaniambia jumaa hayuko ametoka.so tulienda tulipofika jumaa nae akawa ndio anaingia mama akatukaribisha vizuri famili inafurai mume alifurai kuona familia inafuraha.nilipokua nimeketi mume wangu akawa ana ni kumbatia ya kawaida tu kunishika mabega kama kwenye hii picha.tulimaliza kula jumaa akaondoka kama 1hour hivi hatukujua ameenda wapi.akaja na rafiki yetu mwengine but aliporudi alikua ananuka bagi sana.yule rafiki akamwambia mume wangu naomba kumuiba nyota dakika kumi hivi mume wangu akasema sawa.but juma nae akamvuta mama bedroom mimi nikaitwa nje.kufika nje yule mdada akawa ananiambia huyu mzungu amekupenda sana mpaka amekuja kenya hapa mahari paka itoke nikaona kama mchezo.kurudi ndani nikamkuta mume wangu amekasirika amenipiga jicho baya ame turn red nikamuuliza unanini mbona gafla umegeuka? Akaniambia you know.nikamuuliza i know what? Akasema call a taxi we go to the hotel i want to book the next flight to home tmr yani anataka kurudi nyumbani kwao. nikamuuliza what is the problem yeye akashikilia you know.nikamuita juma na mama nikamuuliza kuna nini mbona huyu kageuka? Akanijibu hivi.NIMEMWAMBIA UKIJA KUONA FAMILI LAZIMA UTOE 200K NIMEMWAMBIA ATOE TENA MWAMBIE ATOE AMA NITAMPOKONYA SIMU WALLET YAKE SAA NA KILA KITU ALICHO NACHO.nikamwambia haya yameanzia wapi.nikamwambia mama mama haya mambo gani? Ama akasema mwambie atoe pesa mimi nasimama na jumaa.taxi ilikuja tulipanda tukaondoka.mume wangu alikua ananiambia kumbe hunipendi kumbe ni pesa munataka mumepanga na familia yako muchukue pesa zangu.Imagine.

Jiulize kwanini alikua anasema mimi najua? Kuna game ilichezwa alipotoka akaenda for 1hour.wanivute nje juma amvamie mume wangu.sasa ukiangalia vizuri mimi niko nje sijui kinachoendelea ndani kama mume kavamiwa atoe pesa.kurudi hii picha inakaa kama pia mimi nipo kwenye hio game kabisa couse aliniuliza kwanini umeenda nje wewe.ulijua na mulipanga nyote.basi mume hakutaka kuskiza chochote kwenye taxi nasomewa kama mtoto nabaki kulia tu mimi maana ananilaumu kwakitu sijui.tukafika hoteli aliamua kulala kochini mimi kitandani but kila akiamka ananikuta nalia.mwisho akakubali kua kweli sio wewe ingekua umepanga ata ungelala tu bila kujali.i belive you akaniambia twende kwangu kwa mara ya kwanza tunaenda voi.kisha after 2days tukashuka mombasa mimi na yeye ndio nikaamua kumueka wazi hadharani watu wamjue.so tulikaa miaka miwili but juma alifanya kila njia kututenganisha.aliporudi danmark juma kumbe alimpigia simu akamwambia tuma 200k ama utanijua mimi ni nani.mume hakuniambia but akaniambia after 2months kua ndugu yako alinipigia simu anataka pesa nikamuuliza when akasema 2months ago.mukumbuke mimi na juma hatuongei kwaajili ya hio but juma hata kama mume hakunipenda couse hakufikiria yule zuzu atakua nyota ndogo.tuje kwa harusi sasa hapa ndio mutashangaaaa.na sijawai kuliongea leo ndio nalisema

Leo hii mimi nikaachwa watakao sherekea wa kwanza watakua familia yangu…………..mume wangu alivyokuja vile uwa anakuja for 2weeks akaniambia tumekaa miaka miwili mbona tusioane? Nikamwambia sawa.akasema mwenyewe kesho twende kama mamako nataka kumwambia rasmi kua namtaka mtoto wake.mimi nakamwambia i have to call my brother couse sina baba baba alikufa yeye atachukua nafasi ya baba.nikampigia simu nikamueleza.hata kama tulikua hatuongei but nilimpa heshima yake kama mkubwa wangu couse mimi sinaga madharau…BUT alinijibu hivi.sina mda wakuja kwenye harusi unajua kazi zimepotea na hii tumepata ni kinahati so siwezi kukosesha band kazi kwaajili ya harusi.then nikamwambia but band wanaweza kucheza bila wewe akasema nimeshakwambia siwezi good luck.then after 5min akaandika ujumbe hivi.wewe si ulininunia kwaajili ya kumwambia huyo kibabu wako atoe 200k sina pesa saizi nitumieni 200k nitakuja.sikumjibu.akaona kimya dakika tano zengine akaandika tena ujumbe wangu umeuona ama bado? Siku mjibu.yaliofatia nivitisho.nikakuja kuwavamia kwenye harusi nawaambie vijana wanye kwenye chakula wakojoe tuaribu aribu kila kitu kisha huyu babu nimtie tie makofi.

Tukaenda mpaka kwa mamangu nyumba anaishi mamaangu nailipa mimi kila kitu kilichoko ndani ya nyumba ya mamangu nimekinunua mimi.from vitanda evrything.tulipofika kwa mama mama alifurai kuskia mume anataka kunioa.tukaongea tukayamazima.sote tunajua wazungu hawaonagi kwa mahari.sasa vile anaoa mwafrica lazima tumfunze bila zetu mahari lazima itolewe kuna kilemba waslamu mko wapi.kuma kitu baba upewa na mama pia maiwa but its not maziwa inaweza kua pesa pia but mahari inakuaga ya mschana ndao anapewa ni yake.so mimi nilipoulizwa unataka nini sina makubwa nilisema nataka mamaangu umjengee nyumba simple ya room mbili awe na kwakwe itanipunguzia kulipa hii rent.watu wanasema sijalipiwa mahari? Nikifika home nitawapigia picha ya marriage certificate hapa sifichi kitu.ile nyumba nilianza msingi napesa zangu kwengine kote kajenga mume wangu.kama kuna pesa yangu nimetumia ni 100k pekeake zengine ni mume.so alikamilisha nyumba mamaangu aishi.but kwakua mamangu hakupenda voi hakutaka kuja voi.na mimi sina pesa zakununua land mombasa ni ghali sana.so nikamwambia wacha tuone.mwaka huu mwanzoni tulienda kumtembelea mombasa couse kila akija atasema let’s go to your mum.tulipofika mama akasema mwanaisha nimechoka na mombasa nijengee voi nitaguria huko..tuliangaliana na tatu tukashtuka ni yeye anaongea ama vipi.akasema bora unifungulie biashara nitakaa vou.sindio ikanipa nguvu ya kuongea na mume wangu? Nyumba mliiona toka mwanzo nachimba msingi muliiona.ile nyumba ni mahari yangu kwa mamaangu.

Nyota Ndogo’s confession has left her followers shedding tears with some calling upon her family to settle their indifference and show her love The mother of two went ahead to reveal the main reason she decided to speak out.

 

HII NIA MWISHO.KWANINI NIMEAMUA KUJITOKEZA?

Nimechoka.kila wakati najaribu kusaidia watu wanaona ni haki yao wewe kuwafanyia.sometimes nakosa hata shilingi moja but watoto wengine akiwaomba pesa wao kila mtu sina ama wanamwambia mwambie mwanaisha.ukimuongalia mamangu vizuri hata watoto kama wajukuu hana mapenzi nao vile sana mpaka mbarak anajua.nimekua na watu wamekua karibu na mimi miaka nyingi sana na ukituangalia rangi zetu hatufanani niwaarabu mimi mweusi but they take good care of me na watoto wangu but my family dont like this family but kitu nitawaambia mtu wa nje anaweza kufa na wewe kuliko familia yangu.mume wangu alikua kenya last month for 2weeks akapeleka hio nyumba mbio sana mpaka ilipofikia.mama akasema hawa samaki nachukua kidogo kidogo ningepata friza ingesaidia ningechukua wengi.mume wangu siku yapili bila kuniambia chochote akaniambia twende town nikamuuliza kufanya nini? Akaniambia twende tu nipo nakitu nataka kukuonyesha.mume akaniambia umchagulie mamako friza atakayo.nikachukua nzuri tu garama yake sio nyingi 50k tukampelekea nyumbani yani alifurai sana.siku yapili nikatumana samaki wengi sana.wakajaa kwa friza.kwakweli watu wanapenda samaki wake.nimeona nyumbani nimemfanyia atakavyo nyumba japo haijaisha but yupo ndani.huko nyumbani nasikia amemaliza samaki wamekula pesa zote hawapesa ya kuoda samaki mama anasema anataka kurudi mombasa voi hakuezi.mimi nasjiaje baada yakumfanyia hayo yote.ile nyumba ya mama nilijipatia time imesimama na maji ninayoteka mimi.nilipeleka maji na gari langu mpaka nyumba ikasimama mwenyewe nikilala nalala kama punda.watoto wao wanasomesha mimi kila kitu hata shule kukiwa na shida naitwa mimi.watu walijaribu sana kumpiga mamaangu picha kwa anavyojiweka kishida but sijui why hawakuzitoa.leila mwenyewe kuna time alitaka kupeleka watu wampige mamaake mzazi picha inichomee mimi picha bila kusahau ni mamake.so juma yupo na leila ki team hawa wawili uofia maisha yangu kwakweli.

Munakumbuka wakati alikua akinitukana kwa mitandao.nilikua voi.akinitukana vile alikua na mamaangu.nilitumana ma C.I.D munajua wale simu yako ikiwa on watakupata mpaka ulipo.C.I.D moja alinipigia simu akiniambia hatuezi kumshika mamaako analia sana kua huyu ni mtoto wake hakuna mahali ataenda.sasa ameshawaambia watu hanipendi ananichukia sana yani hanipendi kabisa.ashamwambia mpaka tatu ililimwanaisha nalichukia na moyo wangu wote.leila nimeshampa pesa haziesabiki afanye biasha karibu sijui mara ngapi.biasha ikianguka anakuja ukimwambia sina nitatukanwa nakuwaambiwa na ringa.i want this to stop.mama akitaka kurudi arudi tu mimi nimechoka jamani nimechoka wapenzi siwezi tena.mukinuona mamangu amejitupa yupo rafu mujue nikujitakia musimlaumu nyota tumeongea tumechoka ata vitu analetewa na mume wangu anauza mpaka shuka za kulala ukimuuliza tulikua na nja.jamani njaa gani.mimi mamangu ananitesa moyo wangu sana nampenda maana ningekua simpendi wala nusinge mfikiria siku hizi zote.nafkiri ni wakati wa dada zangu kubeba watoto wao wachangamke watoto wao wasome sio mimi kila kitu.nitasaidia nikijiskia sio lazima couse inakua to much.hawa watoto mpaka kuvaa nguo zakushindia ni mimi niwachukue niende nao sikoni mtumbani mama zao wapo tu.nimechoka jamani NATANGAZA POPOTE MUTAKAPO MUONA MAMAANGU ALIVYO MUSINILAUMU HAJATUPWA ANEJITUPA.