Hivi Ndio Makanga Wa Nairobi UJibu Abiria

Hivi Ndio Makanga Wa Nairobi UJibu Abiria

443

 

Kama hujawahikaa Nairobi,haya ndio majibu utapata kutoka kwa makanga wa huku ile siku utakuja

Njeri: Roysambu ni ngapi?

Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis: Hii gari haina watu bana.

Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.

Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?

Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?

Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis: Ruaka ni how much?

Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger: Shukisha dere.

Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.

Makanga: Basi shuka upande fridge.